Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kuhusu mialiko ya kidijitali, WhatsApp, QR check-in na michango.
Kwa ujumla
Smart Event Pass ni nini?
Ni mfumo wa Kitanzania wa mialiko ya kidijitali na usimamizi wa wageni: kadi za mialiko kwa WhatsApp na SMS, RSVP, QR check-in mlangoni na ufuatiliaji wa michango ya harusi na sherehe.
Mnapatikana wapi?
Ofisi yetu iko Makuburi, Makoka, Dar es Salaam. Tunahudumia matukio kote Tanzania. Simu/WhatsApp: +255 754 380 297, barua pepe: info@smarteventpass.co.tz.
Ni matukio gani mnahudumia?
Harusi, send-off, Kipaimara, sherehe za kuzaliwa, mahafali, mikutano na matukio ya makampuni.
Mgeni anahitaji app?
Hapana. Mgeni anafungua link ya mwaliko wake kwenye simu kama ukurasa wa kawaida.
Naanzaje?
Jaza fomu ya "Tuombe Huduma" kwenye ukurasa wa mwanzo au tuandikie WhatsApp, na timu yetu itakuandalia event yako.
Bei yake ni kiasi gani?
Bei ni kwa kila mgeni: Self-Scan TSh 1,500, With Scanners TSh 2,000, Complete TSh 3,000. Mfano: wageni 200 × TSh 1,500 = TSh 300,000. Angalia vifurushi vyote kwenye ukurasa wa Bei, au tuandikie WhatsApp +255 754 380 297.
Kadi za Mialiko za Kidijitali
Kadi ya mwaliko ya kidijitali ni nini?
Ni kadi ya mwaliko inayotumwa kwa simu (WhatsApp au SMS) badala ya kuchapishwa. Kwa Smart Event Pass kila mgeni anapata kadi yenye jina lake na link ya mwaliko wake binafsi.
Mgeni anahitaji kupakua app?
Hapana. Mgeni anafungua link kwenye simu yake kama ukurasa wa kawaida wa mtandao.
Mnahudumia sehemu gani?
Tuko Dar es Salaam na tunahudumia matukio kote Tanzania, kwa sababu mialiko inatumwa mtandaoni.
Mialiko ya Harusi
Naweza kutuma mialiko ya harusi kwa WhatsApp?
Ndiyo. Kila mgeni anatumiwa kadi yenye jina lake kwa WhatsApp, pamoja na link ya mwaliko wake.
Mnasaidia pia michango ya harusi?
Ndiyo. Mfumo unafuatilia ahadi na malipo ya michango, unatuma vikumbusho na risiti, na kutoa ripoti kwa kamati.
Wageni wanathibitishaje kuhudhuria?
Kwenye link ya mwaliko kuna vitufe vya kuthibitisha (RSVP), na wewe unaona majibu yao kwenye dashboard.
Mialiko ya Send-off
Send-off na harusi zinaweza kuwa kwenye mfumo mmoja?
Ndiyo. Kila sherehe inakuwa event yake, na unaweza kusimamia zote kutoka akaunti moja.
Naweza kuwatumia wageni ujumbe wa shukrani baada ya sherehe?
Ndiyo. Mfumo una kitufe cha kutuma shukrani kwa wageni wote baada ya tukio.
Mialiko ya Kipaimara
Kadi ya Kipaimara inaonyesha nini?
Familia inayoalika, jina la anayepata Kipaimara, jina la mgeni na idadi ya walioalikwa, tarehe, ibada, tafrija na mstari wa Biblia.
Naweza kuchagua rangi ya kadi?
Ndiyo. Kuna miundo zaidi ya kumi ya kadi za Kipaimara yenye rangi tofauti.
Michango na Ahadi
Wanakamati wanaweza kuona michango?
Ndiyo. Kuna portal ya kamati inayowaonyesha michango na matumizi kulingana na ruhusa walizopewa.
Vikumbusho vinatumwa vipi?
Kwa SMS au WhatsApp, kwa ratiba unayoweka, vikiwa na kiasi cha ahadi, kilicholipwa na salio.
QR Check-in ya Wageni
Mgeni akisahau simu yake?
Mhakiki anaweza kumtafuta kwa jina, namba ya simu au Pass ID.
Inahitaji intaneti?
Ndiyo, simu ya mhakiki inahitaji intaneti ili kuthibitisha pass kwenye mfumo.
Mialiko kwa WhatsApp na SMS
Ujumbe unatoka namba gani?
Mialiko ya WhatsApp inatumwa kupitia akaunti rasmi ya biashara ya Smart Event Pass.
Mgeni asiye na WhatsApp?
Anaweza kutumiwa SMS yenye link ya mwaliko wake.
Sherehe na Matukio Mengine
Mnahudumia makampuni?
Ndiyo. Tunasimamia mialiko na usajili wa wageni kwa mikutano, uzinduzi na matukio ya makampuni.
Tuandalie tukio lako
Tuambie kuhusu tukio lako upate bei na ushauri. Tunahudumia matukio kote Tanzania.