+255 754 380 297info@smarteventpass.co.tz

Mialiko ya harusi ya kidijitali

Waalike wageni wa harusi yako kwa kadi nzuri za kidijitali. Kila mgeni anapokea kadi yenye jina lake, link ya mwaliko yenye ratiba ya ibada na sherehe, ramani ya ukumbi, dress code na countdown hadi siku ya harusi. Siku ya sherehe, wageni wanahakikiwa mlangoni kwa QR code.

In English

Digital wedding invitations

Personalised digital wedding invitations for Tanzanian couples: each guest gets their own card and link with the church and reception schedule, venue map, dress code, RSVP and a QR pass that is scanned at the entrance. Save-the-date cards and wedding pledge (michango) tracking are available too.

Unachopata

  • Majina ya maharusi na mgeni

    Kadi inaonyesha majina ya bwana na bibi harusi pamoja na jina la mgeni.

  • Ibada na sherehe

    Tarehe, saa na kumbi za ibada na reception, kila moja na ramani yake.

  • Save the Date

    Tuma taarifa ya awali kabla ya mwaliko kamili.

  • QR check-in mlangoni

    Wageni walioalikwa tu ndio wanaingia, na unaona idadi waliofika moja kwa moja.

Jinsi inavyofanya kazi

  1. 1

    Tupe majina ya maharusi, tarehe, ibada na ukumbi wa sherehe.

  2. 2

    Chagua muundo wa kadi na pakia orodha ya wageni.

  3. 3

    Wageni wanapokea kadi zao kwa WhatsApp au SMS na kuthibitisha kuhudhuria.

  4. 4

    Siku ya harusi, timu ya mlangoni inascan QR za wageni.

Bei kuanzia TSh 1,500 kwa mgeni

Self-Scan TSh 1,500 ยท With Scanners TSh 2,000 ยท Complete TSh 3,000

Ona vifurushi

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Naweza kutuma mialiko ya harusi kwa WhatsApp?

Ndiyo. Kila mgeni anatumiwa kadi yenye jina lake kwa WhatsApp, pamoja na link ya mwaliko wake.

Mnasaidia pia michango ya harusi?

Ndiyo. Mfumo unafuatilia ahadi na malipo ya michango, unatuma vikumbusho na risiti, na kutoa ripoti kwa kamati.

Wageni wanathibitishaje kuhudhuria?

Kwenye link ya mwaliko kuna vitufe vya kuthibitisha (RSVP), na wewe unaona majibu yao kwenye dashboard.

Bei yake ni kiasi gani?

Bei ni kwa kila mgeni: Self-Scan TSh 1,500, With Scanners TSh 2,000, Complete TSh 3,000. Mfano: wageni 200 ร— TSh 1,500 = TSh 300,000. Angalia vifurushi vyote kwenye ukurasa wa Bei, au tuandikie WhatsApp +255 754 380 297.

Huduma nyingine

Tuandalie tukio lako

Tuambie kuhusu tukio lako upate bei na ushauri. Tunahudumia matukio kote Tanzania.